Jinsi ya Kuomba Nafasi ya Kujiunga St. James Kilolo Secondary School
Jinsi ya Kuomba Nafasi ya Kujiunga St. James Kilolo Secondary School
St. James Kilolo Secondary School inapokea maombi ya wanafunzi wanaotaka kujiunga na Kidato cha Kwanza na Kidato cha Tano. Mzazi au mlezi anaweza kuanza mchakato wa maombi kwa kusoma vigezo, kujaza fomu husika na kutuma taarifa kupitia WhatsApp ya shule.
Kabla ya kuanza maombi, hakikisha mwanafunzi anakidhi vigezo vya kujiunga na una taarifa muhimu kama majina kamili, matokeo, shule aliyosoma na mawasiliano ya mzazi/mlezi.
Hatua kwa Hatua za Kuomba Nafasi
1
Soma vigezo vya kujiunga
Hakikisha mwanafunzi anakidhi vigezo vya kujiunga na St. James Kilolo Secondary School kabla ya kujaza fomu.
2
Chagua fomu sahihi
Kama mwanafunzi anaomba Kidato cha Kwanza, tumia Application Form. Kama anaomba Kidato cha Tano, tumia Joining Form Five.
3
Jaza taarifa za mwanafunzi
Weka majina kamili ya mwanafunzi, taarifa za mzazi/mlezi, shule aliyosoma, matokeo na mawasiliano sahihi.
4
Lipa gharama ya fomu kama imeelekezwa
Baada ya kufanya malipo, mzazi anatakiwa kuhifadhi risiti au pay-in-slip kwa ajili ya uthibitisho.
5
Tuma taarifa WhatsApp
Baada ya kujaza fomu, tuma taarifa kupitia WhatsApp ya shule. Kama umelipa fomu, tuma pia picha ya risiti kwenye WhatsApp hiyo hiyo.
6
Subiri mawasiliano kutoka shule
Uongozi wa shule utapitia taarifa zako na kuwasiliana na mzazi/mlezi kwa hatua inayofuata.
Links Muhimu za Maombi
Bonyeza link sahihi hapa chini kulingana na aina ya maombi unayotaka kufanya.
Joining Form One
Joining Form Five
Vigezo vya Kujiunga
Taarifa za Ada
Fomu na Matokeo
Wasiliana WhatsApp
Ushauri kwa Mzazi/Mlezi
Hakikisha taarifa zote unazojaza ni sahihi. Tumia namba ya simu inayopatikana muda wote ili shule iweze kukutumia taarifa za hatua inayofuata kwa urahisi.