VIGEZO VYA KUJIUNGA NA SHULE
Vigezo vya Kujiunga na Shule
Soma vigezo, taratibu na taarifa muhimu kwa mwanafunzi anayetaka kujiunga na St. James Kilolo Secondary School.
Vigezo vya Kujiunga
Kidato cha Kwanza
Vigezo vya Msingi
- Mwanafunzi awe amemaliza Darasa la Saba.
- Awe na ufaulu kuanzia daraja A, B au C.
- Awe tayari kufanya mtihani wa kujiunga kama shule itakavyopanga.
- Awe tayari kufuata sheria, taratibu na maadili ya shule.
Kidato cha Tano
Vigezo vya Msingi
- Mwanafunzi awe amemaliza Kidato cha Nne.
- Awe na ufaulu wa Division One, Division Two au Division Three.
- Awe na ufaulu unaokidhi mchepuo anaotaka kusoma.
- Awe tayari kufuata mfumo wa shule, nidhamu na ratiba za kitaaluma.
Shule ina nafasi kwa wanafunzi wa bweni, wavulana na wasichana. Udahili huzingatia ufaulu, nidhamu, nyaraka sahihi na nafasi zilizopo.
Nyaraka Muhimu Zinazohitajika
Kwa Kidato cha Kwanza
- Nakala ya cheti cha kuzaliwa.
- Nakala ya matokeo ya Darasa la Saba au uthibitisho wa kuhitimu.
- Picha za passport size.
- Risiti au uthibitisho wa malipo ya fomu.
- Application Form iliyojazwa kikamilifu.
Kwa Kidato cha Tano
- Nakala ya cheti cha kuzaliwa.
- Nakala ya matokeo ya Kidato cha Nne.
- Nakala ya school leaving certificate kama ipo.
- Picha za passport size.
- Joining/Application details zilizojazwa kikamilifu.
Hatua za Kuomba Nafasi
1. Soma VigezoHakikisha mwanafunzi anakidhi vigezo vya kujiunga.
2. Jaza FomuJaza application form ya Kidato cha Kwanza au Kidato cha Tano.
3. Lipa FomuLipia fomu kama maelekezo ya shule yanavyoelekeza.
4. Tuma TaarifaTuma fomu au taarifa kupitia WhatsApp ya shule.
5. Subiri MajibuShule itawasiliana na mzazi/mlezi kwa hatua inayofuata.
Viungo Muhimu
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara
Je, shule inapokea wavulana na wasichana?
Ndiyo. St. James Kilolo Secondary School inapokea wanafunzi wavulana na wasichana.
Je, shule ni ya bweni?
Ndiyo. Shule ina mazingira ya bweni kwa wanafunzi.
Je, mwanafunzi wa Division Three anaweza kuomba Kidato cha Tano?
Ndiyo, anaweza kuomba kama ufaulu wake unakidhi mchepuo anaotaka kusoma na nafasi zipo.
Je, mzazi anaweza kutuma taarifa kupitia WhatsApp?
Ndiyo. Mzazi anaweza kujaza fomu mtandaoni na kutuma taarifa kupitia WhatsApp ya shule.
Unahitaji Msaada wa Udahili?
Kwa maswali kuhusu kujiunga, fomu, ada au nafasi za wanafunzi, wasiliana nasi kupitia WhatsApp.
Wasiliana WhatsApp